We were unable to load Disqus. If you are a moderator please see our troubleshooting guide.

Daniel_Mutani • 9 years ago

Mama haelewi hata kama hukuchukua na mali ya wizi ikakutwa kwako na wewe unaonekana unaushirika na mwizi. Kwa kuwa hukuhusika na fedha imeonekana ni ya wizi ushauri wangu kwako ni kurudisha fedha hiyo, pili omba radhi watanzania kwa kuwa huwezi kisema hukushiriki na fedha hizo bado unazitumia..acha kutufanya mazuzu, tumeamka na ukweli naona unaukataa wazi ingawa moyoni mwako unajua. Hutazikwa na chochote marabuondokapo hapa duniani, rejesha fedha hiyo ya maskini...wako ndugu zako wengi wanalala kwenye ngozi na watoto wengi wanaokaa chini na kutembea bila viatu...ona aibu basi

Vincent Akulumuka • 9 years ago

Mmmh!!! sasa ni wazi kwa nini Rais Kikwete ana kigugumizi cha kuwachukulia hatua waliokwapua fedha za ESCROW...sijui ile ahadi ya mwana-TANU (na baadaye ikarithishwa kwa CCM) inayosema ..."Rushwa ni adui wa haki, sitatoa wala kupokea rushwa" nayo imewekwa kwenye freezer kama walivyofanya kwa "Azimio la Arusha"? sijui tunakwenda wapi!!

Hazard • 9 years ago

kweli huyo mama ni balaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!

Muba Muba • 9 years ago

sawa tufanye hujahusika! na sasa umeshajua pesa ulizopewa zimeibiwa na wenyewe walioibiwa unawajua na wewe ni mtu mwema kweli mama hata una shule ambayo watoto masikini hawagusi hata ukuta wake, basi unaonaje kama ukiwarudishia wenye hela zao nawe ukabaki na sifa ya kuwa mtu mzuri mno uliegundua zawadi uliyopewa ni ya wizi na ukairudisha kwa aliyeibiwa.

Be Fair • 9 years ago

Mama una hatia kama hao wengine ni kweli hukuhusika moja kwa moja lakini unazo bilioni 1.6 katika akaunti/shule yako, inaweza kuwa ulikuwa hujui kama kuna ufisadi katika hizo hela wakati unazawadiwa na kaka .. lakini baada ya PAC kudhibitisha ufisadi ulitakiwa uzirudishe halafu ulete hii story ya huna hatia labda tungekuelewa.

Prof Chinchi • 9 years ago

Ni hatari sana ...

joe • 9 years ago

Huyu mama naona ingawa ni msomi haelewi maana ya uwajibikaji .Yeye kama waziri na msimamizi mkuu wa wizara yake na uamuzi wowote utolewayo na wizara yake ,yeye ndiye muhusika mkuu,hivyo kama wizara imeboronga na yeye kama kiongozi mtendaji mkuu anapaswa kuwajibishwa.Ina maana atafukuzwa kazi na afunguliwe mashitaka,kama mh. rais akishindwa kumwajibisha ,basi rais ajaye 2015 aanze kuwawajiobisha hawa walio ktk scandal ya ESCROW!!

Ali MTSASHIWA • 9 years ago

Walituhumiwa wana kila haki kwamba wao ni "..innocent until proved guilty by Court of law ..." Anna stick to this undiluted moral principle .Vipi yeye akubali ni mkosa kwa sababu ya shinikizo au uchunguzi wa wanasiasa wa kamati ya Wabunge ambao ni shida kwa wao wote wewe ni objectivelly neutral kuhusu hili saga la sakata rushwa na uchotwaji wa hela . Waliohutumiwa wapelekwe Mahakamani na sheria stahiki zichukuwe mkondo wake .,Bunge la Taifa si Mahakama.Mapendekezo yabaki kuwa ni mapendekezo tu.Nchi haiwezi kutawaliwa kwa whims na ushabiki wa kila leo wa vyma kisiasa au shinikizo za Mabalozi wapotoshi ambao wanaingilia mambo ya ndani ya Tanzania - kwa sababu ya misaada yao ambayo inayo masharti hata kuhalalisha Ushoga na Usagaji pamoja na ndoa watu wa jinsi moja .Watu kama hao hawaitakii amani na haki Tanzania .

dida • 9 years ago

docile, mtu usiye jua haki zako na familia yako, unasubiri sheria ifanye kazi wakati yunaona kwa uwazi kabisa wanasheria wanachukua rushwa, au wanaenda mahakamani kuzuia bunge lisijadili Escrow, mimi nathani nyie wana sheria justice hamjui mnajua sheria tu tena kwa kukariri kama bibble .you never analyse, au hata kama muna analyse busi mnaamua for your own interests. kwa ufupi hoja zako hazi na mashiko- mama aende zake - hakuumbwa kuwa kiongozi . viongozi wazuri wapo na ni wengi ya kutosha,

Chibunduki, T.T. • 9 years ago

Usimtetee mhaya mwenzio. kupokea hizo hela ni kinyume na maadili ya uongozi. Iwee! upo?

Allan • 9 years ago

She is trying to seduce the President

josephat • 9 years ago

safi sana mama tibaijuka nimeipenda kula kwa nafasi n mda wako sasa inakua vip unashida na pesa then ipo ushindwe tumia hata kama si shule ungekula tu nani hana mdomo wa kula ama tuanze fichua yao

masingiriri • 9 years ago

Wengi tunaamini kuwa ukiwa Profesa, unakuwa na uelewa mkubwa kuliko watu wengi ambao hawakufikia level yako. Lakini huyu mama mbona hivyo ! Michango ya aina yeyote ile, iwe madawati, ujenzi wa vyoo mashuleni, kujenga majengo ya shule n.k. huanzishiwa akaunti kwanza ili hiyo michango iingizwe humo. Hela za Escrow 1.6 Bln ziliingizwa kwenye akaunti yake ! Halioni hilo?

Ruta D • 9 years ago

Mama anashauriwa vibaya. Dhamana aliyo nayo ni ya kisiasa. Kupokea pesa kutoka kwa watuhumiwa maana yake rushwa. Ni rushwa ili kwenye uamuzi uwakingie kifua. Zingatia unaingia baraza la mawaziri. Jambo lingine pima kiasi cha hela hicho, hata kama ni mchango! Kwenye historia ya nchi hii bado nilikuwa sijasikia mchango wa hiari wakiasi hicho. Je, ulilipakodi ulipopokea hela hizo? Je, tunaweza kuona kamtumizi yake katika shule?

Wanduwambo • 9 years ago

Huyu mama na wenzake shuruti aondoke! Kwani mpaka ukamatwe ukiiba ndio ukiri? Kwa kiongozi wa ngazi ya juu wa serikali kama waziri, akituhumiwa hata kwa jambo ambalo anadhani siyo mshiriki "step down" kulinda hadhi yako na elimu pia. Nashindwa kuamini, watanzania watajifunza nini kwa sisi prospective professors!

Obiere Kanga • 9 years ago

Prof. ni cheo kikubwa ktk fani ya usomi na inaonyesha unavyoweza kuchambua mbalimbali kwa upeo mkubwa. Huyu prof haelewi nini maana ya dhana ya uwajibikaji. Kama kweli fedha aliyopewa ni ya shule kwanini asingemwomba mtoaji amwandikie cheki au ahamishe kwa kutumia tis kwenda kwenye A/C ya shule bila kuingizwa kwenye a/c yake. Kuna kitu kipo nyuma ya pazia anachojivunia kwamba huo mgao na wakubwa zake walipata hivyo watamlinda. Asijifiche kwenye kivuli cha shule ukweli upo wazi amechukua fedha chafu! Tujiulize zaidi msaada wa 1.66 bil unakwenda kwa mmiliki wa shule moja kuna shule ngapi ambazo zina matatizo mfano shule za kata hazina maabara, ofisi za waalimu, baadhi ya madarasa hayajakamilika nk. Hayo sio matatizo? Tuache kudanganyana, inaelekea anapata maslahi makubwa sana kwenye uwaziri!

lila • 9 years ago

mwizi huyu mama.mwizi gani atasema kuwa yeye ni mwizi ata akipelekwa mbele ya jaji bado atasema tuu kuwa yeye siyo mwizi ni sisi wanachi tumwondowe na tumfikishe mahakamani na apelekwe jela miaka hamsini na arudishe fedha zetu..rais hatafanya lolote kwa kuwa wanakula kwenye sahani moja tuu.lini tumeona rais amemfuka waziri au kiongozi nchi tanazania au kwenye historia ya tanzania.

Abuu Karata • 9 years ago

HIVI UTAJISIKIAJE MAMA UMESIMAMA MBELE YA WATU AMBAO HAWANA HATA VIATU Hata pesa ya kujitibu, na wewe una mamifuko ya pesa.
Nadhani unastahili kupigwa mawe mama.
Sijui nadhani unajibaraguza tena una moyo kufesi waandishi wa habari lakini nadhani unatamani ardhi ipasuke.

Abuu Karata • 9 years ago

Mama una aibu mbili, aibu ya ndani ya nchi na aibu ya nje, Kwakweli mama nilikuadimire sana, lakini nakuona huna thamani, unaweza kuwa na hayo mbilioni lakini, lalini ni aibu hutaisahau maishani mwako, najua utaachia ngazi tu, ni swala la wakati, Kuachia ngazi haina mana umefanya ni uwajibikaji tu.
Na pia bilioni hizo ziliingia kwenye account yako sio ya shule, kama unavyodai.
Ondoka mama, ni aibu na umemdhalilisha Bank moon

MKOMBOZI • 9 years ago

WAKO WAPI WASHAURI WENYE HEKIMA WAISAIDIE HII SERIKALI IWATENDEE WATANZANIA HAKI.ULIMWENGU UNANGOJEA.

Sandinistas • 9 years ago

This is a very disgusting statement. Ni vigumu kuamini kuwa kauli hii inatoka kwa Prof. Tibaijuka; mtu ambaye tulipata kumheshimu akituwakilisha katika mashirika ya Umoja wa Mataifa. Kwa hakika mimi naamini huyu mama anaelewa vizuri sana kuwa kitendo cha yeye kupokea fedha chafu kwa nafasi yake ni kashfa tosha. Ila pengine anaamini Watanzania ni mbumbumbu hawaelewi kitu na pia anajiamini kuwa yeye ni mtu muhimu sana kwa nchi hii; 'indispensable'. Nadhani pia maneno ya Mama Tibaijuka ni mwendelezo wa tatizo ambalo limeanza kukua sasa la kiburi cha kisomi (intellectual arrogance) hasa miongoni mwa wanasiasa wetu Maprofesa! Au pengine mama Tibaijuka anaamini mamlaka ya ueuzi wake iko poa 'haina neno' na yeye kupokea mihela kutoka kwa matajiri. Mama Tibaijuka akae akijua kuwa wapo Watanzania wengi ambao hawakubali kuona Waziri wao waliyempa dhamana ya kuwatumikia anapokea mihela kutoka kwa matajiri, eti kwa nia njema. Ajue kwamba tafsiri yetu ni kuwa anaitumia ofisi ya umma kama jukwaa la kukusanyia mitaji kwa ajili ya miradi yake binafsi. Tafsiri nyingine ni kwamba amepokea rushwa. Kama anadhani amepata ufadhili, sisi raia tuna uhakika kuwa atalipa fadhila hiyo kwa kutumia ofisi ya umma. Kwa kifupi, kauli yake kuwa hana kosa inaudhi. Mama Tibaijuka anawadharau Watanzania; anawaona ni mazuzu. Mama Tibaijuka apishe ofisi ya umma; aende akasimamie shule zake kwa sababu hatutaki kuona ofisi ya umma inageuzwa kuwa pango la wanyang'anyi.

mishipayasimba • 9 years ago

Huyu mama yeye naye ni mdokozi tuu. Ni vigumu sana mtu akupatie shilingi billion moja bila huduma inayoeleweka. Asingekuwa waaziri wa ardhi , lugemalila asingempatia pesa zote hizo eti kuendeleza shule yake ya msingi! Ukweli utajulikana tuu pale mahakama itakapo sema hana hatia na wala siyo yeye kulopoka lopoka. nashangaa sana kuona waandishi wa habari wanamruhusu huyu mama kujiteteea magazetini. Tafadhali waandishi wa habari, hawa wezi wa mali ya umma, waliotajwa na the KK boys(kabwe na Kafulila) wasiruhusiwe kuongea magazetini. Huyu mama katumia ELIMU YAKE KWA HASARA YA WOTE!

SMN • 9 years ago

Mama vyombo husika vitakusafisha ... kama huna kosa husiwe na wasiwasi jambo moja tu linategemewa UWAJIBIKAJI. Jawabu la haraka lingekuwa kurudisha pesa hizo kwa mwenyewe. Mungu akuongoze.

FRANK • 9 years ago

Safi sana mama tibaijuka,mimi nakuona kama mwanamke shujaa Tanzania na bara zima,endelea na mampambano juu ya ukombozi wa elimuya wanawake,Tanzania ni vipofu mbona Dunia nzima inajua hilo?SWEEDEN wamekuchangia ma pesa kibao katika harakati zako na hawajaonesha hata dalili ya shaka juu yako ,wa Tz kweli tumechoka kuibiwa lakini tusiwavae wasio husika Jame alitoa mchango wa shule na tumtie moyo kama vijana asikatishwe tamaa na kelele hizi azidi kusaidia jamii hii kama wafanyavyo wengine akina Mengi,wewe piga kazi dunia ina kuelewa na sisi vijana tumesha elewa sasaivi wala hatuna mashaka na wewe SONGA MBELE MAMA JEMBE LA AFRIKA,hakuna kutikiswa kidogo tu eti ujiudhuru kwa kupokea mchango wa shule anae sema ivyo ana wivu sana,mama kikwete anazo shule ngapi nani anajua michango ya kuziendesha shule izo ina toka wapi???tuache uonevu hizi taasisi bila kuwa na watu imara hata kumshawishi mtu kuchangia wala sio kitu kidogo na watu wafanya biashara pia wanawaangalia watu wanao waamini ndio wanasaidia kupitia kwao

MASSIMO BOTTELLI • 9 years ago

Mwananchi andikeni maoni ya watu. Mimi ndio nasema Serekali ipunguze hawa kina mama katika Mawizara maana tunapata mashaka na elimu zao pengine ni elimu za kununua na kugushi. Kwani mheshimiwa Lowasa alipochukua hatua za kujiuzulu aliwaambia Watanzania anahusika na RICHMOND au aliona kujisafisha kuwa ni msafi ni kupisha watu wamchunguze. Unakuwaje Profesa na hujielewi. Hebu mheshimiwa JK apishe watu makini wafanye kazi huyu Mama Profesa feki. Alafu nyie CCM acheni kufanya kazi kiundugu na kulindana lindana ndio maana Watanzania hatuwaamini tena. Utawala kutokea Ikulu mpaka mjumbe wa nyumba kumi ndugu tu mtawajibishana vipi ndugu zangu Duh!

Nkwazi .N Mhango • 9 years ago

Dada maji yameishamwagika. Ili ueleweke angalau ungeeleza hiyo fedha nyingi kiasi hicho ni malipo ya nini? Kumbe huoni kosa wakati ukujia wazi umepokea fedha ya wizi? Hiyo PhD yako ni ya kazi gani kama huwezi kujua vitu rahisi kama hivi? Ulinusurika kwenye kashfa ya mjengo wa uhindini kuua watu hapa huponyoki. Kimeumana. Fedha uliyopewa ni ya wizi tu taka usitake. Pia unachofanya ni dharau kwa Bunge, kamati yake, rais hata watanzania wote mliowaibia. Nenda Tibaijuka Nenda. Nenda usingoje kuzomewa wala kupigwa chini nenda tu. Imetosha nenda. Ulipaswa kumshukuru Mungu kwa vile ulipaswa kuwa lupango ukingojea jaji atoe hukumu kwa wizi na uhujumu wa fedha za umma. Shukuru Mungu Kikwete amekuwa mshirika mzuri wa wizi wa fedha za umma kiasi cha kushikwa kigugumizi kuwachukulia hatua.

musa KALOMBA • 9 years ago

Hii inatatizo kubwa sana la maadili hivyo siwezi kushangaa kwa huyu kuongea maneno y kejeli hadhalani wakati akijua ana kosa na kama alikuwa na hoja angeongea bungeni wakati mjadala na sio wakati huu. Mimi ninachokiona ni jeuri ya pesa ya ESCROW na haya ndio malipo ya kuzoea kuchakachua bcoz naamin wabunge wangekuwa makini wakati wa kupitishia katiba ya tume ya warioba hasa sura ya tatu inayohusu miiki na maadili ya utumishi wa uuma huyu mama angekuwa amepigwa chini na huku uchunguzi ukiendelea lakin hawa wezi ndo haohao waliopitisha hiyo katiba na sasa tunavuna tulichopanda. Ila hukumu iko palepale Mungu atafanya yake